Saturday, June 11, 2016

#HABARI NACTE

Chuo cha mifugo na kilimo mbeya kufungiwa,,,


Mkurugenzi wa chuo hicho, Bwana Ellerto Mwamasika
Akisoma uamuzi huo kwa niaba ya NACTE, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla amesema kuwa taarifa kutoka NACTE zinaonesha kuwa chuo hichi kina mapungufu mengi ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya mifugo ambayo hayajathibitishwa na vyombo husika vya serikali.
Pia amesema kuwa chuo hicho kimekuwa kikidahili wanafunzi wasiokuwa na vigezo, akitolea mfano wanafunzi wanaosoma kozi ya mifugo ambapo kati ya wanafunzi 359 ni wanafunzi 89 pekee ndiyo wanaotambulika kuwa na vigezo husika.
Wakizungumza kwa uchungu baadhi ya wanafunzi wamelalamikia chuo hicho kwa kuwasababishia upotevu wa muda na gharama, ambapo baadhi yao walikuwa tayari wamehitimu na walikwenda chuoni hapo kufuatilia vyeti.
“Mimi nimetoka mbali, nimekuja kufuatilia cheti change, sasa nina miezi miwili hapa, kila siku nazungushwa nazungushwa, kumbe walijua wanakuja kufungiwa, kwahiyo cheti change sipati, namuda nimepoteza, nimekaa hapa miaka mitatu halafu leo naambiwa miaka yangu mitatu haina maana tena, sikubali sikubali..” amesema mwanafunzi Catherene Buda huku akitokwa na machozi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa chuo hicho Ellertoni Mwamasika, ameomba radhi na kusema kazi ya kuendesha chuo ni ngumu “Chuo kinawaomba radhi wote, ila mjue kuwa kazi hii ya kuendesha chuo ni ngumu”
Hata hivyo serikali imesema wanafunzi wenye sifa watahamishiwa katika vyuo vingine huku ikimuagiza mmiliki wa chuo hicho kuwalipa wanafunzi gharama zao zote kabla hawajatoka chuoni hapo.

No comments:

Post a Comment