Sunday, June 12, 2016

Ufafanuzi kuhusiana na makato ya pesa kuanzia tarehe 1 jully kweny simu na mabenki kwenda TRA



Watu wengi wamestuka sana kusikia kuwa kuanzia tarehe 01 Julai 2016, kila utakapotoa fedha kwenye ATM au huduma za fedha kwa mitandao ya simu, TRA itachukua asilimia 10 ya pesa hizo.

Ukweli ni kuwa kodi hiyo ya 10% kwenye muamala wa simu au kutoa pesa kwenye ATM itakatwa kwenye gharama ya kutolea au kutumia na wala siyo kwenye pesa zako.

Mwanamtandao Gabriel Mwang'onda amefafanua kuwa 'kwa mfano ukitoa sh milioni moja gharama ya kutolea ni sh 7500,  basi serikali wanakata 10% kutoka katika hiyo sh 7500 (sh 750) na siyo kwenye sh milioni moja'.


No comments:

Post a Comment